Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeshiriki katika Monesho ya tatu ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya EPZ mkoani Geita. Katika maonesho hayo TBA inaonyesha bidhaa na huduma zinazotolewa na Wakala. Banda la TBA lilitembelewa na Wakuu wa Wilaya za Biharamulo na Nyang’hwale na kupata maelezo juu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA katika Mkoa wa Geita na maeneo mengine.