Mnamo Julai 17, 2022 Waziiri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amefungua rasmi jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambalo limekamilika kwa asilimia 100
Ujenzi wa jengo hilo umetekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kama Mkandarasi na Mshauri Elekezi na kugharimu takribani shilingi bilioni 1.331.
Jengo hilo lina Ofisi 19, ukumbi mmoja wa mikutano, jiko na stoo.