Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefaya ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita unaotekelezwa na TBA kama Mkandarasi na Mshauri Elekezi. Akiwa katika eneo hilo la Mradi amefurahishwa na kasi ya ujenzi huo na kuipongeza TBA kwa kuendelea kutekeleza mradi huo katika ubora wa hali ya juu.
Pia Waziri Ummy amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli
kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo na miradi mingine ya
Afya kote Nchini.
Vile vile kipekee ameipongeza TBA kwa kuendelea kutekeleza miradi
katika kiwango cha juu. Aliongeza pia kwa kumpongeza Meneja wa TBA Mkoa wa
Geita Mhandisi Gladys Jefta kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha
ujenzi unakwenda vizuri.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Eng. Robert G. Luhumbi ameipongeza TBA kwa kazi nzuri
iliyofanyika katika ujenzi wa hospitali hiyo huku akimpongeza meneja wa TBA na
wasaidizi wake. Vile vile Mhe. Mkuu wa Mkoa ameshukuru Mhe. Rais. Dkt. John
Pombe Magufuli kwa kuleta mradi huo wa hospitali kwani utasaidia kuokoa maisha
ya wanawake wengi wakati wa kujifungua pamoja na wagonjwa wengine watakaopata
huduma katika hospitali hiyo ya Rufaa.
Meneja wa TBA Mkoa wa Geita Mhandisi Gladys Jefta amemshukuru Waziri
wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa kutembelea mradi ya Afya ambao unatekelezwa na
TBA kwa mfumo wa buni - jenga (Design & Build). Aliongeza pia kuwa
amefarijika sana kuona Waziri ametambua kazi inayofanywa na TBA kuwa ni yenye
ubora na ameahidi kuyafanyia kazi yale yote ambayo Waziri ameagiza.
Aidha Mhandisi Gladys amempongeza Mhe. Rais. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwekeza kwenye Sekta ya Afya.