WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO ARIDHIKA NA KASI YA UJENZI KATIKA MRADI WA MAGOMENI KOTA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack
Kamwelwe ametembelea mradi wa Makazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam na
kuridhishwa na kasi ya Ujenzi wa mradi huo unaojengwa na Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) ambao unatarajiwa kukamilika Juni 30, 2020.
Mhe. Waziri amefanya ukaguzi wa mradi huo kuanzia maeneo ya nje mpaka ndani, hivyo kujionea maendeleo ya mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa umeweza kufikia hatua nzuri. MWaziri unatarajiwa kutoa makazi kwa kaya 644 na kubakiwa na makazi mengine 12 ya ziada kutokana na kuongezeka kwa gorofa moja