WANANCHI WAKARIBISHWA KUTEMBELEA BANDA LA TBA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), unashiriki maonesho ya wiki ya utumishi wa umma kwa mwaka 2024 kwa lengo la kutoa elimu juu ya huduma inazotoa.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu inayosema kuwekeza kwa utumishi wa umma uliojikita kwa umma wa Afrika karne ya 21 iliyojumuishi na inayostawi ni safari ya mafunzo na mabadiliko ya Kiteknolojia, yanafanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma
Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu, Mkurugenzi wa Huduma Saidizi TBA, Bw. Mathias Mhembe, amesema maonesho hayo yanalenga kuonesha safari ya mabadiliko katika mifumo ya Teknolojia ambayo TBA ni sehemu ya mabadiliko hayo, akitolea mfano mifumo ya Kidijitali ambayo TBA inatumia kama vile mfumo wa malipo (MUSE), mfumo ya utendaji kazi, mfumo wa mishahara na mifumo mingine ya mawasiliano ya kiofisi.
Kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TBA, Bw. Mhembe ametumia nafasi hii kuwakaribisha wananchi na watumishi wote wa umma kutembelea Banda kuona kazi zinazotekelezwa na TBA.
Maonesho haya ni ya wiki nzima ambayo yatamalizika tarehe 23 Juni, 2024.