• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • English

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaWakala wa Majengo Tanzania

  • kuhusu Sisi
    • Ujumbe kutoka kwa Mtendaji Mkuu
    • Sisi ni Nani
    • Dira na Dhamira
    • Tunafanya Nini
    • Mikakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Bodi ya Ushauri
    • Muundo wa Taasisi
    • Senior Management
    • Kurugenzi wa Uwezeshaji wa Huduma
    • Kurugenzi ya Ushauri
    • Kurugenzi ya Ujenzi
    • Kurugenzi ya Miliki
    • Meneja wa Mikoa
  • Nyumba
    • Nyumba za Kuuza
    • Nyumba za Kupangisha
    • Fomu ya Ununuzi wa Nyumba
    • Fomu ya ununuzi wa Nyumba
  • Miradi
    • Miradi Tunayoishikilia
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyo Katika usanifu
    • Miradi Tunayotegemea kufanya
  • Machapisho
    • Machapisho
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
  • Ununuzi
    • Mpango wa Manunuzi wa Mwaka
    • Mialiko ya zabuni
    • Orodha ya Wazabuni Walioshinda

Habari Mpya

  • SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWENYE UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI

    tokea mwezi 1
  • MENEJIMENTI YA TBA YAHIMIZWA KUKUTANA MARA KWA MARA.

    tokea miezi 2
  • TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

    tokea miezi 2
  • TBA NA ZBA KUENDELEZA MASHIRIKIANO

    tokea miezi 2

Latest Press Release

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI MAGOMENI KOTA

Imewekwa: Monday 23, March 2020

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI MAGOMENI KOTA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za Makazi Magomeni Kota Machi 16, 2020 unaotekelezwa na Wakala wa MajengoTanzania (TBA). Mradi huo unaotekelezwa na TBA kama Mkandarasi na Mshauri Elekezi, utakapokamilika unatarajiwa kutoa makazi kwa kaya 644 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 70% na unategemewa kukamilika mwezi Juni, 2020.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Selemani Kakoso (Mb) amesema kuwa kamati imeridhishwa na kazi inayofanywa katika kutekeleza mradi huu na ameipongeza TBA kwa ubunifu wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata zege na kiwanda cha kufyatulia matofali kama njia ya kupunguza gharama za utekelezaji wa mradi.

Pia Mhe. Selemani Kakoso ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) kuipa fedha TBA kiasi cha bilioni 14 ili mradi huu uweze kukamilika kwa wakati. Vilevile, ameiomba Serikali kuipa TBA vibali vya kuajiri ili kukabiliana na upungufu wa wataalam 300 uliopo kwa sasa ili kuiongezea ufanisi wa kutekeleza miradi nchini.

Akizungumza katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (Mb) amesema wataalam kutoka Wizarani watafika Alhamisi ya 19 Machi, 2020 kufanya uhakiki wa gharama zilizotolewa na TBA kujiridhisha na kiasi cha fedha kinachohitajika kukamilisha utekelezaji wa mradi huo na kuitoa mara moja pamoja na kuendelea kufuatilia kwa ukaribu mwenendo wa utekelezaji wa mradi huu.

Akiongea katika ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema TBA imeshaandaa mpango kabambe kwa ajili ya kuendeleza eneo la Magomeni Kota ambapo awamu ya kwanza imehusisha ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya kaya 644. Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa majengo ya kupangisha pamoja na majengo ya kutolea huduma kwa wakazi watakaokuwa wakiishi katika eneo hili.

Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

TBA
THE CHIEF EXECUTIVE, TANZANIA BUILDINGS AGENCY (TBA), 13 MOROGORO ROAD, P.O BOX 94, 41102 VIWANDANI, DODOMA TANZANIA, EMAIL: ce@tba.go.tz Website: www.tba.go.tz
Nukushi :
Namba ya Simu : +255 733 483 437, +255 677 108 010
Barua Pepe : barua@tba.go.tz

Linki za Haraka

Linki Linganifu

  • WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Utumishi
  • Tume ya Takwimu ya Taifa
  • Tume ya Ajira

©2025 wakala wa majengo tanzania . Haki zote zimehifadhiwa..

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.Inaendeshwa na Wakala ya Majengo Tanzania