Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha S. Amour ametembelea na kukagua Mradi wa Nyumba za Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika ziara hiyo Balozi Aisha alisema amekagua na kujiridhisha kuwa mradi huo umekamilika kwa Asilimia 100 na kuwa nyumba hizo zimejengwa kisasa kulingana na mahitaji ya sasa. vile vile Balozi Aisha ametoa rai kwa watakao kuwa wakazi wa mradi huo kuzitunza vyema kwani Serikali imetumia gharama nyingi katika kutekeleza mradi huo.
kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kondoro amewahakikishia wakazi hao kuwa utaratibu uliotumika kufanya uhakiki wa wakazi hao ulikuwa shirikishi na hivyo wakazi wote watapata fursa ya kurudi katika nyumba hizo.