Katibu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. Joseph Kilangi pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) walifanya ziara maalum ya kutemebelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA katika Mkoa wa Dodoma. moja ya miradi iliyotemebelewa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma 3500 ambapo kwa awamu ya kwanza zitajengwa nyumba 150. Mradi huo unaoendelea kujengwa katika eneo la Nzuguni B Dodoma.