Katika Maonesho ya 25 ya Nanenane mkoani Simiyu, watu wengi walivutiwa na Banda pia huduma iliyokuwa inatolewa na TBA kwenye maonyesho hayo. Miongoni mwa viongozi na watu mashuhuli waliotembelea Banda la TBA ni pamoja na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Dkt. Raphael Chegeni (Mb); Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) na Waziri wa Kilimo Mstaafu Dkt. Titus Kamani.
Wote
walipongeza kazi kubwa inayofanywa na TBA katika sekta ya Ujenzi na huduma ya
nyumba inayotoa kwa watumishi wa umma. Katika Banda la TBA kulikuwa na Picha na
michoro ya miradi mbalimbali inayotekeleza katika mkoa wa Simiyu na Kanda ya
ziwa kwa ujumla.