Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula (Mb) ametembelea banda la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika maonesho ya nanenane yanayoendelea kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mhe. Dkt.
Mabula amesema TBA ni taasisi kongwe hivyo bado itaendelea kutegemewa na
Serikali katika kusanifu, kushauri na kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo
ambayo itakuwa na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande mwingine, Mhe. Dkt. Mabula amefurahishwa na mradi unaosimamiwa na TBA wa Ujenzi wa soko la kisasa la mnada wa mifugo unaoendelea eneo la Buzilayombo, wilayani Chato, Mkoani Geita. Mhe. Dkt. Mabula amesema kukamilika kwa mradi huo kutatatua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufungua soko rasmi la mifugo na kuongeza kipato kwa wananchi na Serikali kwa ujumla. Vile vile ametoa rai kwa TBA kuendelea kujiimarisha zaidi kwa kuongeza jitihada zaidi katika kutekeleza majukumu yake.