Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Umma kutoa huduma bora kwa wananchi huku akizitaka Taasisi zote za Umma kuhuisha Mikataba ya Huduma kwa Mteja kwani ni nyenzo na kiungo muhimu katika kuboresha utendaji kazi kati ya Serikali na Wananchi inaowahudumia.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 23, 2023 wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshirikikwenye Uzinduziwa Mikataba ya Hudumakwa Mteja ya Taasisi za Umma katikaKilele cha Maadhimisho ya Wiki yaUtumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mhe. Simbachawene amewataka Watumishi hao kutambua kuwa wanapotoa huduma bora kwa wananchi wanamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza suala hilo mara kwa mara.
Kufuatia hatua hiyo, amezitaka Taasisi za Umma kuzingatia Mikataba ya Huduma kwa Mteja katika utoaji wa huduma kwa wananchi ili haki na wajibu wa pande zote mbili utendeke kwa watoa huduma na wapokea huduma ambao ndio wateja. Ameongeza kuwa Ofisi yake ina wajibu wa kusimamia mifumo na viwango vya utendaji kazi Serikalini kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na moja ya mifumo na viwangovya Utendaji Kazi huo ni Mkataba wa Huduma kwa Mteja.
Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ni moja ya hatua muhimu ya kuboresha huduma bora kwa wananchi ambapo amesema jumla ya Mikataba ya Huduma kwa Mteja Taasisi za Umma imeweza kuzinduliwa."Uzinduzi wa mikataba hii ya Huduma kwa mteja inakwenda kuwezesha watumishi wa umma kuwa na utamaduni wa utendaji kazi unaojali matokeo na tija kwa wakati" amesema Mkomi
Aidha, Katibu Mkuu Mkomi ametumia fursa hiyo kuzipongeza Taasisi za Umma ambazo zimeadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye maeneo yao kama ilivyoelekezwa na Ofisi yake.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daudi Kandoro akitoa neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa mikataba hiyokwa niaba ya Wakuu wa Taasisi, amesemawatatekeleza maagizo yote yaliyotolewa huku akiahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kilichoandikwa katika mikataba hiyo ili wananchi waweze kujua wajibu na haki zao.