Imeelezwa kuwa Mpango wa manunuzi ni nyenzo muhimu katika kutekeleza kazi za manunuzi za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kondoro alipokuwa anafungua kikao kazi cha maafisa manunuzi wa TBA ambao wako jijini Dodoma kuandaa mpango wa manunuzi wa TBA wa mwaka 2024/25.
Kondoro amesisitiza kuwa, kikao kazi hicho ni muhimu katika kujadili kwa uwazi mpango huo kwa lengo la kufanikisha shughuli ya manunuzi kwa weledi na ufanisi mkubwa.
"Mpango wa manunuzi huu mtakaojadili ni Dira ambayo itasaidia kuleta ufanisi mzuri wa kazi za manunuzi za Wakala"
Awali akimkaribisha Mtendaji Mkuu, Mkurugenzi wa Huduma Saidizi (DBS), Bw. Mathias Mhembe ametaja kuwa asilimia zaidi ya 70 ya Bajeti ya Taasisi ni Manunuzi hivyo mpango huu, utaweka Dira ya jinsi ya kufanya manunuzi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria.
Jumla ya washiriki 53 wanahudhulia Kikao kazi hicho ambacho kinafanyika katika ukumbi wa TBA Dodoma