Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Geita umekamilisha nakukabidhi rasmi miradi ya ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbogwe zilizopo mkoani Geita. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nyang’wale ilikabidhiwa Januari 31, 2023 huku Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe ikikabidhiwa Februari 2, 2023.
Majengo ya ofisi hizo yalibuniwa na ujenzi wake kusimamiwa na TBA kama Mshauri Elekezi.