TBA KUANZA AWAMU YA PILI YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeanza awamu ya pili ya
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Mbeya. Awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa msingi pamoja na kusimamisha nguzo
wa majengo. Awamu hii ya pili ni muendelezo wa majengo haya mawili makubwa ya
ghorofa yaliyosimama kwa takribani miaka mitatu kwa kukosa fedha.
Awali mradi huu ulikua chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya ambapo kwa sasa utasimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Ujenzi huu utajumuisha jengo la upasuaji na utakasaji
vifaa (CSSD) pamoja na jengo la wodi la upasuaji. Kukamilika kwa ujenzi huu
kutaboresha utoaji wa huduma hizi ambazo hazina miundombinu hii kwa sasa.
Wizara imeshasaini mkataba na kwa sasa maombi ya fedha pamoja na nyaraka zote
muhimu ya kuanza ujenzi yamewasilishwa Hazina kwa utekelezaji.
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ni taasisi ya Serikali
iliyoanzishwa mwaka 2002 kwa lengo la kusimamia miliki za Serikali.