Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeendelea na ujenzi wa nyumba 3500 katika eneo la Nzuguni B jijini Dodoma ikiwa ni hatua ya kupunguza uhaba wa nyumba kwa watumishi mbalimbali waliohamia huko. Mradi huo mpaka sasa zimejengwa nyumba 102 kati ya nyumba 150 zilizopangwa kujengwa awamu ya kwanza.