Mji wa Serikali ambao ujenzi wake umesimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), umezinduliwa rasmi Aprili 13, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amepongeza Taasisi zilizoshiriki kufanikisha ujenzi huo.
Akitoa maelezo kwa Mhe. Rais kuhusu Mradi huo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA Daudi
Kondolo, alisema Ujenzi wa Mradi huo hadi kukamilika kwake umezingatia ubora
kwa kuweka Miundombinu yote inayostahili kwa ikiwemo pia ya watu wenye ulemavu.
Aidha Mtendaji Kondolo amebainisha kuwa Majengo yote yaliyojengwa
katika Mji huo yako imara na yanakidhi
viwango vinavyotakiwa.
Katika Mradi huo, TBA ilipewa jukumu la ubunifu wa majengo
pamoja na kusimamia ujenzi huo kama Mshauri elekezi kwa kusimamia Wakandarasi
wote walioshiriki ujenzi wa Mji huo.
Pamoja na kusimamia pia TBA imeshiriki kujenga Jengo la
Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora kama moja ya Wakandarasi, sehemu ambayo
uzinduzi huo ulifanyika.
Mambo yaliyozingatiwa katika Ubunifu wa Majengo hayo ni
pamoja na mahitaji ya Walemavu, matumizi makubwa ya mwanga asilia katika
Jengo, muonekano wa kisasa wa
Jengo, mahusiano baina ya Ofisi moja na nyingine, ukubwa wa nafasi, upepo asilia katika jengo,
usalama wa Jengo na watumiaji kama uwepo
wa Vizima Moto na Vifaa vya
kutambua uwepo wa moto na Maegesho ya magari kwa Wakuu wa Wizara, Watumishi na
Wageni