Ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ulioanza kutekelezwa katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma unaendelea kwa kasi huku ukitarajiwa kukamilika kwa wakati. Ujenzi huu unaosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unatarajia kukamilika Juni 2024, kwa gharama za kiasi cha shilingi Bilioni 29
Akizindua ujenzi huo hivi karibuni, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima alihimiza kazi ifanyike vizuri na kukamilika kwa wakati ili kuwezesha wahusika kuanza kulitumia jengo hilo kwa wakati.
“Nawahimiza TBA wasimamie vizuri ili kazi ifanyike vizuri na wamalize kwa muda uliopangwa. Nahitaji kuona ubora wa kazi ili jengo lionekane zuri na la kisasa, zaidi kwenye madirisha, milango, sakafu na rangi iwe yakuvutia”. Alihimiza Dkt. Dorothy