UONGOZI
WA MKOA WA SONGWE WARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA
NA TBA
Uongozi
wa Mkoa wa Songwe umeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa
na TBA mkoani humo. Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David
Kafulila na Bi. Regina Bieda Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma. Mhe.
Kafulila ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Songwe linalojengwa eneo la Mselewa Wilayani Mbozi, ujenzi wa jengo la
Hospitali ya Wilaya ya Tunduma, pamoja na ujenzi wa jengo la ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.
Mhe.
Kafulila amesema kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo ni kubwa kinyume na
matarajio ya ofisi yake na amethibitisha kuwa TBA inafanya kazi nzuri sana mkoani
Songwe achilia mbali changamoto kadhaa zilizojitokeza hasa suala la fedha
kutoka katika ofisi yake ya Mkoa.
Vile
vile Mhe. Kafulila amepongeza jitihada na ushirikiano mkubwa unaotolewa na TBA mkoani
Songwe katika kusukuma kasi ya utekekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa
katika Mkoa huo.
Aidha,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Bi. Regina Bieda amesema
anatambua jitihada zinazoendelea kufanywa na TBA Mkoa wa Songwe kuwa zimezaa
matunda hasa katika kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa ya
maendeleo. Pia, amepongeza utendaji mzuri na ushirikiano mkubwa wa TBA Mkoa wa
Songwe na kuonesha nia ya kuendelea kufanya kazi na Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA).
Naye Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Arch. Steven Simba amesema, ofisi yake inajukumu kubwa la kuendelea kutekeleza kwa wakati miradi yote iliyochini ya TBA katika Mkoa wa Songwe kwa kuzingatia ubora, muda wa mkataba na gharama nafuu