Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeanza awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya. Awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa msingi pamoja na kusimamisha nguzo wa majengo.
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wapongezwa kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo Mkoani Tabora. Uongozi wa Mkoa wa Tabora ulitoa jukumu kwa TBA kusimamia na kujenga miradi ya maendeleo kwa ubora na viwango vinavyohitajika katika majengo mbalimbali mkoani humo.
TBA itaendelea kuwa Taasisi imara kutekeleza Miradi kwa ubora
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Philis M. Nyimbi ameupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ametembelea mradi wa Makazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya Ujenzi wa mradi huo unaojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao unatarajiwa kukamilika Juni 30, 2020.