Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umetekeleza miradi mbalimbali Mkoani Mbeya. Miradi iliyotekelezwa inajumuisha miradi ya Ujenzi, Ushauri na ukarabati.
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unashiriki kama Mshauri Elekezi Msaidizi (Sub-Consultant) katika utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha mpakani mwa Tanzania na Malawi unaoendelea katika eneo la Kasumulu, Mkoani Mbeya.
Uongozi wa Mkoa wa Songwe umeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na TBA mkoani humo. Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Mhe. David Kafulila na Bi. Regina Bieda Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za Makazi Magomeni Kota Machi 16, 2020 unaotekelezwa na Wakala wa MajengoTanzania (TBA).
KAMATI YA BUNGE YA MIUNDO MBINU YAIPONGEZA TBA